• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 5:55 AM
TAHARIRI: Kaunti zitafute mbinu za kujitegemea kifedha

TAHARIRI: Kaunti zitafute mbinu za kujitegemea kifedha

KITENGO CHA UHARIRI

SUALA la kucheleweshwa kwa fedha za kaunti limekuwa tatizo ambalo halijatafutiwa ufumbuzi.

Muda si mrefu uliopita, shughuli katika kaunti zote zilikaribia kusimama kwani Seneti haingeweza kukubaliana juu ya mfumo wa ugawaji wa fedha.

Kulikuwa na sherehe wakati msuguano huo uliisha lakini yaonekana furaha hiyo ilikuwa ya muda mfupi.

Wanaotatizika zaidi kifedha ni wafanyikazi wa kaunti, ambao bado wanasubiri mishahara yao ya Septemba na Oktoba. Kwa kawaida, magavana hushutumu Hazina ya Kitaifa kwa kuchelewesha pesa. Sababu hasa inaweza kuwa nini?

Haitakuwa busara kwa mamlaka ya Hazina ya Kitaifa kuendelea kukawia, kisha baadaye kutoa fedha hizo.

Ni dhahiri kwamba serikali ya kitaifa inajitahidi kutafuta pesa.

Na kama tulivyosema hapo awali, suluhisho la kudumu ni kaunti kukoma kuetegemea ufadhili wkutoka kwa serikali ya kitaifa. Ucheleweshwaji wa fedha hizo hupelekea mkwamo wa shughuli na utendakazi wa kaunti, jambo linalotilia shaka uwezo wa baadhi ya kaunti kujitegemea kifedha.

Ni muhimu kwamba kaunti zitafute mbinu na rasilimali za kuzisaidia kumudu mahitaji yake ya kifedha kwa kuunda sheria zitakazozisaidia kuafikia malengo hayo.

Baadhi ya kaunti zimeonyesha kuwa kushirikiana na kaunti jirani kuweka pamoja rasilimali zao kunaweza kuwaweka pazuri kifedha na kumaliza mtegemeo kwenye serikali kuu kwa ufadhili.

Kwa mfano, kaunti za pwani zaweza kuungana kupatiliza rasilimali za bahari na utalii.

Kulingana na mwenyekiti wa Baraza la Magavana Wycliffe Oparanya, magavana wana wasiwasi mkubwa juu ya kucheleweshwa kwa pesa.

Sio tu mishahara, bali kaunti pia zimesitisha utekelezaji wa bajeti na miradi ya maendeleo huku utoaji wa huduma ukidhoofishwa.

Walakini, kaunti pia zimekumbwa na kashfa tele za ufisadi na usimamizi mbaya wa rasilimali. Uovu huu lazima ukomeshwe.

You can share this post!

Trump azimwa

ONYANGO: BBI: Uhuru, Raila wasikilize rai za wakosoaji