• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:50 AM
Uchunguzi wa kifo cha Tecra Muigai kufanyika Februari

Uchunguzi wa kifo cha Tecra Muigai kufanyika Februari

Na RICHARD MUNGUTI

OMBI la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) la kutaka uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha Tecra Muigai, bintiye mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe cha Keroche usikizwe Mahakama ya Lamu liligonga mwamba Jumanne.

Hakimu mkazi Bi Zainab Abdul aliamuru uchunguzi huo ufanywe Nairobi kuanzia Februari 24 2021.

Uamuzi huu uchunguzi ufanyiwe katika mahakama ya Milimani Nairobi umesitisha makinzano na mabishano makali kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jina (DCI) kule uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha Tecra wapasa kufanyiwa.

DPP alitaka uchunguzi ufanyiwe Lamu naye DCI alitaka ufanyiwe Milimani Nairobi akisema mashahidi wakuu wote wako Nairobi.

Akitoa uamuzi, hakimu mwandamizi Bi Zainab Abdul alisema mashahidi wengi watakaotoa ushahidi katika uchunguzi huo wanaishi Nairobi na haifai ufanyiwe mahakama ya Lamu.

Bi Abdul alitupilia mbali ombi la DPP kwamba uchunguzi huo ufanyiwe mahakama ya Lamu ambapo Tecra anadaiwa alianguka na kupata majeraha kisha akasafirishwa hadi hospitali ya Nairobi Hospital alikolazwa siku chache kabla ya kuaga.

Kabla ya kupata majeraha yaliyopelekea kifo che, Tecra alikuwa amechumbiana na Bw Omari Lali , muhudumu wa mashua za kuwabeba watalii katika bahari hindi.

Tecra anadaiwa alianguka na kupata majeraha kisha akasafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu maalum.

Ripoti ya upasuaji ilionyesha alikuwa amepata majeraha kichwani. Aliaga baada ya siku chache.

Lali alikamatwa na kuzuiliwa kwa mauaji ya Tecra kisha mahakama ya Lamu ikamwachachilia ikisema “hakuna ushahidi wa kutosha kuwezesha Lali kushtakiwa kwa mauaji ya Tecra.”

kufunguliwa mashtaka ya Lali wa kuwezesha shtaka la mauaji kufaulu.”

Lali aliachiliwa miezi miwili iliyopita kisha DCI akaamuru kisha uchunguzi wa kubaini ju

Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) Geoffrey Kinoti alikuwa akitaka uchunguzi huo ufanyiwe mahakama ya Milimani Nairobi.

Mkinzano kati ya DPP na DCI kuhusu mahala Cuchunguzi huo utakapofanyika ulichelewesha kusikizwa kwa mashahidi katika mahakama ya Milimani.

DPP na DCI wamekuwa wakionyesha ubambe katika uchunguzi huo. Wazazi wa Tecra walimwandikia DCI barua wakiomba uchunguzi ufanyike Nairobi.

Walisema wanaishi Nairobi na mpasuaji maiti mkuu wa serikali aliyechunguza maiti ya Tecra anahudumu kutoka Nairobi.

“Mashahidi wakuu katika uchunguzi huuu wanaishi Nairobi. Hakuna haja uchunguzi huu uendelezwe mjini Lamu,” alisema Bi Abdul.

“Nakubaliana DCI kuwa wazazi wa marehemu na mashahidi wanaishi Nairobi na sio Lamu,” alisema Bi Abdul.

You can share this post!

Majopo 15 yaliyoundwa na Rais yavunjwa na mahakama

Je, nini maana ya ugonjwa wa sciatica?