Chifu mtumizi wa Twitter afariki
NA FAUSTINE NGILA
Chifu wa Nakuru eneo la Umoja amaarufu kama ‘Tweting Chief’ kutokana na mtindo wake wa kutumia mtandao wa Twitter kukomesha uhalifu, amefameriki.
Familia yake ilisema kwamba alifariki akiwa hospitali ya Nakuru ambapo alikimbizwa alipopata matatizo ya kupumua. Alifariki akiwa na umri wa miaka 55.
“Baba yangu aligojeka Jumanne na tukampeleka hospitali ya Evans Sunrise Nakuru kabla ya kuhamishwa haospitali yaa Nakuru alipofariki alipokuwa akipokea matibabu,” mwanawe Ken Kariuki aliambia Taifa Leo wa njia ya simu.
Mwanawe wa kike alisema kwamba babayake alikuwa amegojeka kisukari kutoka kitambo.
Alitambulika mwaka 2014 kwa kutumia matandao kupigana na uhalifu kwa kutumia matandao wa Twitter.
Bw Kariuki aliongoza jamii ya watu 30,000 huku mtandao wa Twitter akiwa na wafuasi 60,000 na kuna wale waliokuwa wakipokea ujumbe huyo kupitia kwa ujumbe mfupi kwa simu zao.
Kabla ya kifo chake Kariuki alikuwa amepunguza vitendo vya uhalifu kupitia jumbe zake za mtandao wa Twitter.