Habari Mseto

Mimea ya bangi yang'olewa shambani

October 26th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

VITALIS KIMUTAI NA FAUSTINE NGILA

Maafisa wa usalama wameng’oa mimea zaidi ya elfu moja ya bangi katika shamba moja Kipkelion, Kaunti ya Kericho.

Mwanamume wa mika 35 alikamatwa anayeaminika kumiliki mimmea hiyo haramu Alhamisi jioni kwenye msako uliofanya na maafisa wa usalama.

Polisi pia walisema kwamba mashukiwa huyo pia alipatikana na bangi iliyokauka na pia mbegu zake .

“Polisi  kutoka kituo cha Kiplekoin walisema kwamba walipata ripoti kutoka kwa wakati kwamba kuna mtu alikuwa amepanda mme huyo haramu kwenye Kijiji cha Moyoyuet,” alisema polisi.

Kulingana na ripoti kamishena wa kaunti Veronica Musyoka Pamoja na chifu msaindizi wa eneo hilo Felix Ruto na afisa mkuu wa kituo cha polisi wa kituo cha Kipkeloin alienda nyumbani mwa mshukiwa na kufanya uchunguzi.

Bangi  iliyokuwa imekauka ilipatikana nyummbani kwake na bengu zilipatikana mfoki kwake. Mshukiwa huyo alizuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Kipkelion.

Uuzaji wa bangi umekuwa mwingi sana kaunti za Kericho na Bomet huku washukiwa kadhaa wakikamatwa wakiwa na bangi na kushtakiwa, lakini hilo halijakomesha uuzaji wa bangi eneo hilo.

Wanaouza mihadarati hiyo wanalenga wanafunzi wa eneo hilo.