Habari Mseto

Kizaazaa kortini mshukiwa akivamiwa na mwanawe

November 9th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA FAUSTINE NGILA

Kizaazaa kilishuhudiwa kwenye korti ya Bomet Jumatatu asubuhi wakati fundi aliyemchoma mkewe kwa petroli alifikishwa kizimbani.

Robert Kipkorir Tonui alifikishwa mbele ya jaji Roseline Korir na akakana mashtaka hayo.

Kabla ya kufikishwa mbele ya  jaji mwanawe wa kike wa miak 21  alimvamia nje ya korti akitaka kujua kwanini alimuua mama yake.

Bw Tonui anashtakiwa kwa kumuua mukewe Bi Emmy Chepkoech mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Cheptal.

Bi Emmy  alichomwa mwili wote na akafariki huku  akipokea matibabu kwenye hospitali ya Tenwek.

Emmy ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka45 alizikwa kijijini Kobel Oktoba 19 huku akiacha Watoto saba.

Kituko hicho kinaaminika kutendeka Oktoba 7 kijiji cha Konoin.

Tonui alifikishwa kortini akiwa anaandamana na watu wa familia yake na wakazi wwakati alisomewa mashtaka kabla  George Mureithi kutoa ripoti ya uchunguzi wa kiakili ulionyesha kwamba mshukiwa alikuwa na akili sawa.

Bw Tuniu alikana mashtaka hayo huku akiomba kuachiliwa kwa dhamana. Lakini mwendesha mashtaka alipuuzilia mbali maombi hayohuku akisema kwamba Bw Tonui alikuwa kwenye hatari kwani bado hofu bado ilikuwa bado mingi maeneo mauaji hayo yalipotokea.