Habari Mseto

Watu 9 wafariki ajalini Mazeras

November 10th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA MAUREEN ONGALA NA FAUSTINE NGILA

Watu tisa walifariki  Jumapili wakati matatu na lori ziligongana kwenye barabara la Kaloleni-Mazeras eneo bunge la Rabai  Kaunti ya Kilifi.

Mbunge wa Kaloleni  Paul Katana alisema kwamba ajali hiyo ilitokea eneo la Bondora saa tisa jioni wakati matatu iliyokuwa ikielekelea Kaloleni kutoka  Kaunti ya Mombasa iligogana na Lori.

Waaalioathirika walikuwa Watoto wawili na watu wazima saba.

“Ajali hiyo  ilitokea kilomita mbili kutoka mahali nilikuwa  kwenye mpaka wa Kaloleni kuelekea Rabai .Lori hilo na matatu zizligogana kichwa.Miili hio tisa ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Makandara,”Bw Katana aliambia Taifa Leo.

Alisema kwamba walioumia walipelekwa kwenye hospitali tofauti kuokea matibabu.

Mbunge huyo alisema kwamba eneo hilo  limekuwa linatokea ajali nyingi.

“Drivers are always speeding yet there are no bumps,” he said, adding he asked the Kenya National Highways Authority (KeNHA) to act quickly. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Kilifi Stephen Matu alidhibitisha kisa hicho hukuakisema kwamba hakupokea ripoti kamili.