Habari Mseto

Dereva wa miraa ahofiwa kusombwa na maji

November 12th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA WAWERU WAIRIMU na FAUSTINE NGILA

Dereva aliyekuwa akisafirisha miraa anaohofiwa kuwa alifariki baada ya kubebwa na maji kwenye barabra ya Kinna-Garbatulla kufuatia mvua kubwa iliyoshhudiwa eneo hilo.

Hussein Kesane, wa miaka 52 alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Land Cruiser akielekea Kaunti ya Garissa Ijumaa Usiku wakati tukio hilo lilitokea.

Alikuwa akisafirisha miraa kutoka Maua Kaunti ya Meru huku akiwa na mwezake Ibrahim Billow wakati gari hilo liliiingia kwa mmaji kilomita moja karibu na mjiwa Garbatulla.

Wakati gari lilakwama kwenye maji wawili hao waliamua kutoka ndani ya gari ili wajiokoe lakini Bw Billow ndiye alifanikiwa kujiokoa kutokana na mafuriko hayo ambaye baadaye aliripoti kisa hicho  kwenye kito cha polisi cha Garbatulla Kaunti ya Isiolo.

Ripoti za polisi zilisema kwamba akiatu moja na stakabathi za dereva huyo zilipatikana kwenye eneo la tukio.

Kamanda wa polisi wa Garbatulla Alloys Orioki alisema kwamba uchunguzi unaenelea kufanywa  na kwamba timu ianyofanya shunguli hiyo imetafuta kwa ubali wa kilomita kadhaa bila mafanikio.Shunguli hiyo inaendeshwa na maafisa wa usalama  pamoija na wakazi wakisaidiwa na tigatiga.

“Mwili  huo unaendelea kutafutwa na tunaimani kwanmba tutaupata,”alisema Bw Orioki.