Wito amani idumishwe Marsabit
JACOB WALTER NA FAUSTINE NGILA
Polisi wa Marsabit wamewaomba viongozi na wakazi wadumishe amani kufuatia hofu ambayo inashudiwa baada ya mauaji ya mwalimu wa shule ya upili Jumamosi na watu waliokuwa na bunduki.
Bw Jeremiah Ado Hanche mwalimu wa shule ya upili ya Dakabaricha alipigwa risasi mara tano nyumbani kwake Marsabit.
Kamanda wa polisi wa Marsabit Samuel Mutunga alionya viongozi kwamba kuhusiana na kuchochea kati ya wakazi na polisi na akamwaomba wawe wavumilivu ili uchunguzi ufanyike.
Alisema kwamba polisi hawana nia ya kuficha mshukiwa yeyote ambaye alitenda kitendo hicho.
Kumekuwa na kilio kutoka kwa wananchi wakihusisha polisi na tuki hilo .Lakini Bw Mutunga alisema kwamba waliotenda kitendo hicho watachukuliwa hatua bila ubanguzi.
Aliomba mtu yeyote ambaye anaweza kuwa na ujumbe wowote ajitokeze asaindie wapelezi kufanya uchunguzi na kukamaa washuiwa bila woga.
Mkuu huyo wa polisi aliwaonya watu ambao walikuwa wanaandaa maandamano huku wakihatarisha Maisha ya watu wengine.
Alisema kwamba uchunguzi utafanywa na maafisa wakuchunguza uhalifu kutoka kwa kaunti kwani wakazi tayari hawana Imani na polisi.