Habari Mseto

Wezi wa mifugo watoroka na mbuzi 200 Kapedo

November 15th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

FLORAH KOECH NA FAUSTINE NGILA

Majambazi waliokuwa wamejihami wanaoshukiwa kutoka Kaunti ndogo ya Tiaty Jumapili walivamia eneo la Kapedo na wakatoroka  na mbuzi 200.

Mavamizi hayo yalidhibitishwa na kamanda wa polisi wa Kaunti ndofgo ya Turkana Masahriki Edwin Ogwari.

Tukio hilo lilijiri siku moja baada ya zadi ya viongozi  50 kutoka eneo hilo kufanya mkutano wa amani ili kuimiza amani kati ya jamii.

Vamizi hilo la Jumapili asubuhi lilifanywa na wavamizi waliojihami na kuvamia wafungaji kutoka jamii ya Turkana waliokuwa wakilisha mifugo yao mita chache kutoka milima ya Silale.Wavmizi hao walipiga risasi njuu mara mbili kabla ya kuondoka na mifugo hao.

Kulingana na Bw Ongwari hakuna mtu aliyeumiaa kwenye shambulizi hilo lakini  mifugo hao walioibwa walipelekwa eneo la Silale Tiati Masahriki.

“Vamizi hilo lilifanyika assubuhi wakati wafungaji kutoka Kapedo walikuwa wanalisha mifugo wao karibu na mlima wa Silale.Wavmizi hao walipiga risasi mbili njuu ili kuwaogopesha wafungaji na kuiba Zaidi ya mbuzi 200 wakazielekeza Silale Tiati Mashariki,”alisema Bw Ogwari.