• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:50 AM
LISHE: Samaki wa mchuzi

LISHE: Samaki wa mchuzi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 2

Vinavyohitajika

• samaki 2

• vitunguu maji 2

• vitunguu saumu punje 5

• nyanya 4

• mafuta ya kupikia

• juisi ya ndimu

• chumvi

• karoti 2

• tangawizi

• pilipili mboga

Maelekezo

Andaa vitunguu saumu, tangawizi na ndimu.

Tenga kitunguu saumu kwenye sehemu mbili.

Osha na kisha marinate samaki wako – weka tangawizi, vitunguu saumu, juisi ya ndimu na chumvi.

Acha samaki kwenye jokofu ili viungo viingie vizuri.

Menya vitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti na kisha kata vipande vidogo.

Weka mafuta kwenye kikaangio kilicho mekoni. Subiri yapate moto vizuri.

Weka samaki na ukaange hadi aive vizuri. Ukimaliza weka samaki pembeni.

Bandika sufuria, weka mafuta uliyokaangia samaki. Subiri yapate moto vizuri kisha weka vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya kahawia.

Weka pilipili mboga na koroga mchanganyiko.

Weka vitunguu saumu huku ukiendelea kukoroga kuzuia visigande kwenye sufuria.

Weka karoti na endela kukoroga.

Weka nyanya kisha funika kwa muda wa dakika 5. Hakikisha kuwa moto si mkali sana, bali uwe wa wastani.

Kamulia ndimu kwenye mchanganyiko na weka chumvi kisha koroga kiasi.

Weka samaki na ongeza maji kiasi ,jaribu kuandaa mchuzi mzito.

Acha yachemeke. Maji yakikaukia mchuzi wako utakua tayari na unaweza pakua na chochote ukipendacho.

You can share this post!

UNDP kutumia teknolojia kuboresha mazingira ya safari za...

Raha ya wakulima mswada wa chai ukipita bungeni