• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Vifaa butu vyazidi kutemwa huku vipaji vikihifadhiwa KPL

Vifaa butu vyazidi kutemwa huku vipaji vikihifadhiwa KPL

Na CECIL ODONGO

HUKU msimu wa kuingia sokoni na kuwanunua au kuwauza wachezaji ukiendelea, klabu za Posta Rangers na Kakamega Homeboyz zimeanza kuimarisha vikosi vya kupitia usajili mpya huku Wazito FC na Tusker FC wakizidi kuwaachilia wanakabumbu wao.

Posta Rangers wamemsaini kipa mzoefu wa Tusker David Okello na washambulizi Edwin Lavatsa na Paul Odhiambo. Wawili hao walikuwa wametemwa na waunda mvinyo hao kutokana na kushuka kwa  ubora wa viwango vyao.

Hata hivyo Posta wamewaachilia ndugu wawili Peter ‘pinches’ Opiyo na Levis Opiyo pamoja na Geodfrey Kataka ambao sasa wako huru kusaka klabu nyingine za kusakatia.

“Tunafurahi kutangaza kuzitwa huduma za kipa David Okello na washambulizi Edwin Lavatsa na Paul Odhiambo kwa kandarasi itakayodumu kwa muda wa miaka mitatu. Pia tumewaachilia Peter Opiyo, Levis Opiyo na Geodfrey Kataka. Tunawakaribisha wanaoingia na kuwatakia kila la kheri wanaoondoka,”  ikasema taarifa katika mtandao wa klabu.

Huku hayo yakiendelea Mwenyekiti wa Kakamega Homeboyz  Cleophas Shimanyula ametangaza kwamba wamezitwa huduma za mshambulizi wa Nairobi City Stars Jimmy Bageya.

Vijana hao wa kocha Paul Nkata waliofanya kweli katika mchuano wa SportPesa Super Cup kwa kuwaadhibu Yanga ya Tanzania wameazimia kujishughulisha mno sokoni ili kukiimarisha kikosi chao.

“Tumesaini Bageya tunapoimarisha timu kwa mkondo wa pili wa ligi na kulenga nafasi ya tano ligini. Ameshiriki mazoezi kabambe nasi na kocha ameridhika na uchezaji wake,” akasema Bw Cleophas Shimanyula.

Wazito nao wamewachilia wachezaji watano akiwemo straika wao matata Piston Mutamba aliyejiunga na Sofapaka. Hata hivyo hawajalala usingizini baada ya kuwaleta kikosini aliyekuwa kiungo wa Gor Mahia na Sofapaka Erick Ochieng’ na  Edwin Wanjala, Anthony Njeru na Zedrick Imbotsa

You can share this post!

RAMADHANI: Biashara yanoga Mwezi Mtukufu ukifika ukingoni

JAMVI: Ziara za Ruto zageuka siasa za 2022 licha ya...

adminleo