• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Wanafunzi wagoma wakitaka sketi fupi

Wanafunzi wagoma wakitaka sketi fupi

Na KNA

WANAFUNZI wa Shule ya Upili ya Olooseos katika Kaunti ya Kajiado, wamegoma wakitaka kuruhusiwa kuvaa sketi fupi na kusukwa nywele kwa mitindo ya kisasa.

Wasichana hao zaidi ya 270 waliondoka shuleni hJumatatu usiku, jambo ambalo limewatia wasiwasi wazazi wengi.

Wanafunzi hao wanadaiwa kupanga mgomo huo dhidi ya mwalimu mkuu, Farida Maritim, kwa madai ya kutozingatia matakwa yao.

Zaidi ya hayo, wanataka wawe wakila nyama mara tatu kwa wiki, badala ya Jumamosi pekee ilivyo sasa.

Wanafunzi hao, wengi kutoka vidato vya tatu na nne wanadaiwa kutekeleza mpango huo usiku wa manane.

Iliripotiwa kwamba walikuwa wamepanga kuchoma ofisi kuu lakini wakazimwa na walinzi.

Baadaye, mwalimu mkuu aliwaita polisi kutoka eneo la Kiserian iki kusaidia kuimarisha usalama.

“Ilikuwa hali ya kuogogya, ila nashukuru Mungu kwamba hakuna uharibifu wowote uliofanyika. Walichofanya tu ni kuvunja ua na kuondoka bila kuzua mafarakano yoyote,” akasema Bw Marirtim, aliyeonekana mwenye ghadhabu.

Alisema kwamba wasichana wengi ambao waliondoka shuleni humo usiku walikamatwa na polisi katika miji ya Kiserian na Birika.

“Wote wako hapa. Tumeamua waende nyumbani kwa likizo ya kati ya muhula. Hii ni kwa kuwa tungeshindwa kuwadhibiti. Ningetaka kuzungumza na kila mzazi kibinafsi, ili tujue mikakati tutakayoweka kukabili hali hiyo. Haya yanahusu maisha yao ya baadaye, ila si walimu au mimi binafsi,” akasema.

Bodi simamizi wake tayari ishafanya mkutano uliowashirikisha wadau kadhaa wa elimu katika juhudi za kurejesha hali ya kawaida shuleni humo.

You can share this post!

Mwanamke alilia polisi waachilie mume aliyenajisi binti yake

TAHARIRI: Wauzao bidhaa feki ni wauaji, wanyongwe!

adminleo