• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 2:56 PM
Oserian yachunguzwa kwa kuwakandamiza wafanyakazi wa maua

Oserian yachunguzwa kwa kuwakandamiza wafanyakazi wa maua

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya maua ya Oserian inachunguzwa kuhusiana na madai ya kuwalipa wafanyikazi wake kiwango cha chini cha mshahara licha ya kuwa mwanachama wa shirikisho la kimataifa ya wauzaji maua.

Kampuni hiyo inachunguzwa na Fairtrade, shirikisho la Uingereza. Ripoti hii ni kwa mujibu wa Mail on Sunday.

Kulingana na ripoti hiyo, kampuni hiyo inawalipa wafanyikazi wake kiwango cha chini zaidi kuliko gharama ya maisha nchini Kenya.

Kulingana na gazeti hilo Sh12,782 kwa mwezi, mshahara ulio wa chini sana ukilinganishwa na gharama ya maisha.

“Tunachunguza utaratibu ili kujua viwango vya Fairtrade vya ujira na mandhari ya kufanya kazi. Tutatoa taarifa kwa umma baada ya kupata matokeo,” ilisema Fairtrade katika taarifa.

You can share this post!

Rotich arekebisha makosa katika ufadhili wa nyumba za...

Kutanyesha tena, yasema idara

adminleo