• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Kikosi kizima cha polisi chasukumwa jela kwa mauaji

Kikosi kizima cha polisi chasukumwa jela kwa mauaji

Na AFP

OCAMPO, MEXICO

SERIKALI imefunga gerezani kikosi kizima cha polisi cha mji wa Ocampo, Mexico kufuatia mauaji ya mgombeaji wadhifa wa umeya.

Maafisa serikalini walisema hatua hiyo imechukuliwa ili kufanikisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo.

“Wote wanahojiwa kwa msingi wa kisheria kubainisha kama kuna yeyote kati yao aliyehusika na uvunjaji wa sheria,” afisa wa idara ya usalama serikalini katika Jimbo la Michoacan ambako mji wa Ocampo unapatikana akasema.

Mji huo mdogo una idadi ya watu karibu 20,000 pekee. Hata hivyo, haikubainika maafisa wa polisi waliokamatwa ni wangapi.

Mgombeaji umeya Fernando Angeles, aliuawa kwa risasi Alhamisi iliyopita alipokuwa akijiandaa kwa kampeni.

Angeles ni mgombeaji wa tatu wa umeya kuuawa kwa risasi mwezi huu, huku kukiwa na zaidi ya wanasiasa 100 waliouawa tangu kampeni za uchaguzi zilipoanza Mexico.

-Imekusanywa na Valentine Obara

  • Tags

You can share this post!

Pasta aitisha waumini Sh200,000 aombee Nigeria kufuzu

Hamasisho wanaume wavae minisketi

adminleo