• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
RUTH KAMANDE: Mauaji yalitokana na kero rohoni

RUTH KAMANDE: Mauaji yalitokana na kero rohoni

Na WYCLIFFE MUIA

WATAALAMU wa akili wanasema ongezeko la vifo vya kimapenzi nchini linatokana na watu kuwa na matarajio ya juu sana katika mahusiano yao.

Dkt Jane Kiarie, mtaalamu wa masuala ya kiakili anasema kisa cha Ruth Kamande kumuua mpenziwe si jambo ambalo lilitokea ghafla, mbali lilisababishwa na msururu wa mambo ambayo yalikuwa yakimkera mfungwa huyo kwa muda.

“Katika saikolojia tunasema kuwa tabia au kisa kama hicho huchochewa na mambo mengi. Ruth hakuamka tu siku hiyo na kuamua kumuua mpenziwe, kulikuwa na msururu wa mambo ambayo yalimfika upeo,” anasema Dkt Kiarie.

Kulingana na mtaalamu huyo, mahusiano mengi pamoja na ndoa zinaishia kusababisha mauti kwa sababu ya misingi dhaifu ya uhusiano wa wapenzi.

“Ni muhimu wazazi watoe mfano mzuri na kuwashauri watoto wao kuhusu masuala ya mapenzi wanapokua. Vijana wengi wanaingia katika ndoa kwa sababu za kiajabu kuwa mpenzi wao atawapa kile hakupata kwa wazazi wao,” anasema Dkt Kiarie.

Naye daktari wa masuala ya kiakili Dkt Lukoye Atwoli anawashauri wanandoa kuwa makini na hali ya kiakili ya wapenzi wao haswa wakati wanapokosana.

Kulingana na Dkt Atwoli, hisia za watu hupanda zaidi wakiwa katika uhusiano wa kimapenzi kuliko wakati mwingine ule maishani, na ni muhimu kuchukua hatua za haraka ili kuepuka visa vya kuuana.

“Ruth hakuhitaji kuua mpenziwe kwa kumdunga mara 25. Lazima hali yake ya kiakili wakati huo haikuwa ya kawaida,” anasema Dkt Atwoli.

You can share this post!

RUTH KAMANDE: Muuaji mrembo aliyepata ‘A’ KCSE...

Kuria ajuta kumsimanga Raila

adminleo