• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Utumizi wa Kiswahili shuleni wazua ubishi TZ

Utumizi wa Kiswahili shuleni wazua ubishi TZ

Na JOSEPHINE CHRISTOPHER

WATANZANIA wameshindwa kuamua kuhusu lugha wanayofaa kutumia kufunza shuleni kati ya Kiswahili na Kiingereza.

Wataalamu katika kongamano lililofanywa Jumanne waligawanyika, upande mmoja ukitetea Kiswahili huku mwingine ukitaka Kiingereza kitumiwe.

“Wale wanaotetea Kiswahili ni wanafiki. Walisoma ng’ambo na pia watoto wao wanasomeshwa katika shule za Kizungu,” akasema Dkt Michael Kadeghe, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Watetezi wa Kiswahili walisema utumizi wa lugha za kigeni ni sawa na ubeberu wa kilugha.

Prof Marttha Qorro, alisema lugha hiyo hufaidi tu nchi za kigeni, akataka Tanzania ifuate mfano wa Uchina na Japan ambazo huthamini lugha zao za kiasili.

Mjadala kuhusu luha bora zaidi inayopaswa kutumiwa kwa mafunzo nchini humo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka 40 sasa, na wataalamu wa pande mbili za kilugha hawajawahi kuelewana.

Kuna wanaoamini kuwa Kiingereza si rahisi kueleweka kwa Watanzania, lakini watetezi wa lugha hiyo wanasema hakuna lugha yoyote iliyo rahisi kueleweka kushinda nyingine ifikapo katika masomo.

You can share this post!

Polisi mjamzito aua mwanamume kwa kumkejeli

Zanu PF yashinda viti vingi bungeni huku fujo zikianza

adminleo