• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 3:03 PM
Ombi la Gor kusongeshewa mechi KPL lakataliwa

Ombi la Gor kusongeshewa mechi KPL lakataliwa

Na CECIL ODONGO

KAMPUNI inayoendesha ligi kuu nchini KPL imeiambia Mabingwa mara 16 wa KPL Gor Mahia kwamba hawatasongesha mechi yao ya Ijumaa Agosti 17 dhidi ya Chemelil Sugar FC.

Mnamo Jumatano Gor Mahia waliwasilisha kilio chao kwa KPL na kuwaomba wasukume mbele baadhi ya mechi zao ikiwemo ya Chemelil ili kuwapa muda wa kutosha kupiga mazoezi makali kwa ajili ya kipute cha kuwania ubingwa wa Kombe la Mashirikisho Barani (CAF)  dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ugani MISC Kasarani.

Kulingana na raiba iliyotolewa mapema Agosti, mabingwa hao watetezi wa KPL watalazimika kuwajibikia mechi kumi mwezi wa Agosti pekee ili kupunguza mrundiko wa mechi za kuwajibikia katika ratiba yao.

Hata hivyo kocha wa K’Ogalo Dylan Kerr sasa amesema mechi hizo zinaawaathiri vibaya wachezaji wake ongezea kuwapa uchovu mwingi kwa kuwa wanalazimika kusakata mechi tatu kila wiki.

“Tafadhali usimamizi wa KPL unafaa kujua kwamba hatuwezi kucheza mechi tatu kila wiki kwasababu Inaathiri sana kiwango cha uchezaji wa wanadimba wangu,”  akasema Bw Kerr.

Vile vile mkufunzi huyo alisisitiza kwamba KPL inafaa kuzingatia kwamba wanabeba bendera ya Kenya katika mechi za CAF ndiyo maana wanafaa kupata muda wa kutosha kujitayarisha ili kung’aa katika mashindano hayo.

Hata hivyo, akimjibu Afisa Mkuu Mtendaji wa KPL Jack Oguda alisema kwamba itakuwa vigumu kupangua baadhi ya mechi za Gor kwa kuwa msimu wa mwaka wa 2018 unatarajiwa kukamilika mapema kuliko ya mwaka wa 2017.

“Hatuwezi kupangua ratiba za mechi zao tena japo pia hawajatuandikia rasmi barua kulalamikia msongamano wa ratiba. Walitueleza kwamba watasakata mechi ya Chemelil mjini Kisumu na hatuwezi kuairisha mechi hiyo maana Chemelil washajitayarisha,” akasema Bw Oguda.

You can share this post!

Malkia Strikers watakaosaka ubingwa Japan watajwa

Kenya yainyeshea Sudan 4-0 U-17

adminleo