Kimataifa

Polisi Tanzania watisha kukamata kijiji cha watu 1,600

August 17th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

AFP Na PETER MBURU

POLISI nchini Tanzania Alhamisi walitishia kuwakamata wakazi wa kijiji kizima kusini mwa taifa hilo, baada ya watu wengi kuharibu mifereji ya maji.

Wakazi wa kijiji cha Ngolo walidaiwa kuharibu kwa kuikata mifereji hiyo iliyokuwa ikisafirisha maji kuelekea eneo jirani la Mbeya.

Hii ilikuwa baada ya Gavana Albert Chalamila kuamuru kuwa wakazi wote wa kijiji hicho wakamtwe, hata wagonjwa, wazee na watoto mnamo Jumatano.

Baada yake, polisi Alhamisi walituma magari kwenda kuwakamata wanakijiji hao, kulingana na ripoti za kamanda wa polisi eneo hilo, Ulrich Matei.

“Walifanya kosa la kiuchumi. Serikali imetoa pesa za kuwekeza mifereji ya maji kisha wanaiharibu, hatuwezi kukubali hivyo,” akasema Matei.

Mkuu huyo wa polisi alsema alituma magari na polisi wa kutosha kuwakamata wanakijiji hao.

Habari kuhusu kisa hicho bado si wazi, huku kijiji hicho chenye idadi ya watu takriban 1, 600 kikiwa katika eneo kavu.