• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:44 AM
Wakurugenzi wa KICC wamulikwa

Wakurugenzi wa KICC wamulikwa

Na BERNARDINE MUTANU

Ripoti mpya ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali inaonyesha kuwa wakurugenzi wa Jumba la Mikutano la Kenyatta (KICC) walijilipa zaidi ya kiwango kilichowekwa.

Wakurugenzi hao walitumia Sh22.1 milioni katika mishahara na marupurupu katika mwaka wa kifedha wa 2015-2016.

Lakini kiwango kilichoidhinishwa ni Sh14.8 milioni, alisema mkaguzi huyo, Bw Edward Ouko.

Kulingana naye, wakurugenzi hao hawakutoa ithibati kuwa matumizi ya fedha zaidi yaliidhinishwa na bunge kuambatana na sheria.

Wakurugenzi wakuu wa KICC ni pamoja na aliyekuwa waziri msaidizi Omingo Magara, na Nana Gecaga, mpwawe Rais Uhuru Kenyatta.

Nana alikuwa katika bodi hiyo kwa miezi mitatu baada ya kuteuliwa Aprili 1, 2016.

You can share this post!

Nyumba 1,000 sasa zishabomolewa

Mbunge anyakwa na EACC kuhusu ufisadi

adminleo