• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
IPSOS: Kazi yetu ni kutafiti, si kuhukumu wafisadi

IPSOS: Kazi yetu ni kutafiti, si kuhukumu wafisadi

Na PETER MBURU 

SI kazi yetu kubaini nani mfisadi ama nani si mfisadi, ila tunakusanya maoni ya Wakenya kuhusu wanachodhani, ndiyo msimamo wa kampuni ya utafiti ya Ipsos Kenya baada ya kutangaza matokeo ya utafiti kuhusu ufisadi Agosti 22.
Mtafiti Mkuu wa kampuni hiyo Prof Tom Wolf, amesema kazi ya kudhibitisha kuwa mtu ni mfisadi ni ya mahakama na wala si la kampuni yoyote ya utafiti.
Prof Wolf alisema hayo Jumatano, baada ya maoni ya Wakenya kuonyesha kuwa wanasiasa wafisadi zaidi humu nchini ni Naibu Rais William Ruto akifuatwa na gavana wa Kirinyaga Bi Anne Waiguru.
Alisema kuwa Wakenya huunda taswira zao kuhusu ufisadi kutokana na taarifa wanazosoma au kutazama kwenye vyombo vya habari.
“Majina mengine ambayo yametajwa hapa na pale ni maoni ya Wakenya kutokana na ripoti wanazopata kupitia vyombo vya habari. Si maoni yetu,” akasema Prof Wolf.
“Si kazi yetu kumfuata mtu yeyote kutaka kujua ikiwa ana hatia yoyote anapotajwa na asasi za kupambana na ufisadi na kuhojiwa,” akasema mtafiti huyo.

You can share this post!

Mama taabani kukusanya hela za vijana kuwapeleka kazini...

Google sasa yawezesha watumiaji kutuma baruapepe za siri

adminleo