Habari Mseto

Barabara mpya kusaidia kupunguza msongamano jijini

January 21st, 2024 1 min read

NA HILARY KIMUYU

WAKAZI wa Nairobi sasa watafikia katikati mwa jiji (CBD) kwa urahisi baada ya serikali kufungua barabara mpya ya Nairobi Expressway Haile Selassie Exit Plaza, yenye vijia vitano.

Waziri wa Barabara na Uchukuzi, Bw Kipchumba Murkomen, Jumamosi, Januari 20, 2024 alisema ujenzi huo, ulioanza mwishoni mwa Julai 2023, utasaidia sana katika kurahisisha masuala ya usafiri.

“Tunafuraha kutangaza kwamba shughuli ya majaribio ya barabara mpya ya Nairobi Expressway Haile Selassie Exit Plaza iliyokamilishwa imeanza kutumika Jumamosi, Januari 20, 2024,” alisema Bw Murkomen.

Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/habari/barabara-mbovu-zakarabatiwa-jijini-nairobi-miezi-michache-baada-ya-nms-kumezwa

Waziri Murkomen alielezea kuwa kukamilishwa kwa ujenzi wa Barabara ya Nairobi Expressway ni ushirikiano kati ya sekta ya umma na ya binafsi.

“Pia kuna mipango ya kuongeza vijia zaidi,” akasema Bw Murkomen.

Alifichua kuwa katika eneo la Museum Hill, ambalo kwa sasa lina vijia vitatu pekee, mipango inaendelea ya kuongeza vijia zaidi.