Dimba

Arsenal yapewa asilimia kubwa ya kushinda EPL, City ikiwa tishio pekee

Na MASHIRIKA November 4th, 2025 Kusoma ni dakika: 2

LIGI Kuu ya Uingereza (EPL) iko zaidi ya robo kwenye kampeni ya kuwania ubingwa baada ya kila timu kucheza mechi 10 kufikia sasa.

Angalau mshindi mmoja wa taji na vita vya kuteremka daraja atalazimika kufanya kitu ambacho hakuna mtu aliyewahi kufanya.

Arsenal wako kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 25-jambo ambalo ni wastani (24.7) kwa mabingwa wa mwisho kuwa kazo baada ya mechi 10.

Katika misimu 14 kati ya 33 ya ligi hiyo hadi sasa, timu iliyokuwa kileleni katika hatua hii imeendelea kushinda ubingwa.

Lakini ni mara saba tu ambapo timu yenye pointi 19, idadi ya Manchester City walio nafasi ya pili, au 18, amnbazo ndizo Liverpool, Sunderland na Bournemoth walizo nazo, baada ya mechi 10 imeshinda taji hilo.

Hakuna timu iliyowahi kufanya hivyo kwa pointi chache zaidi, jambo ambalo lingewaondoa wagombea wengine wote.

Arsenal wanaongoza City kwa tofauti ya pointi sita, ambapo ndiyo idadi kamili ya pointi nyingi zaidi ambazo timu imewahi kutoka nyuma katika hatua hii na kushinda taji.

Manchester United msimu wa 2002-03 na Manchester City msimu wa 2013-14 ndio timu pekee zilizowahi kushinda taji la EPL baada ya kuwa nyuma ya vinara kwa pengo la pointi sita au zaidi baada ya mechi 10.

Lakini ikiwa unaamini katika ishara, hii inaweza isiwe nzuri kwa The Gunners. Msimu huo, City walifanya hivyo, walikuwa na pointi 19 na Arsenal walikuwa na 25, idadi kamili sawa na msimu huu.

The Gunners waliishia nafasi ya nne jedwalini.

Katika historia ya EPL, hakuna timu iliyowahi kunusurika kushuka daraja baada ya kuwa na pointi mbili tu baada ya mechi 10 ya kwanza.

Kila timu iliyokuwa na rekodiu hiyo mbaya katika hatua hiyo ya msimu hatimaye ilishuka daraja.

Takwimu hii inaonyesha ugumu wa hali hiyo, na kihistoria, kuwa na pointi chache hivyo mwanzoni mwa msimu ni ishara mbaya sana kwa matumaini ya timu kusalia katika ligi hii maarufu, hivyo Wolves ambao wana pointi mbili pekee wamo hatarini.

Nottingham Forest walio na pointi sita, na West Ham (saba), vile vile zimo katika eneo hatari la kushuka daraja.