Ruto, Raila wafika Kasarani kushuhudia Kenya ikilemea DR Congo na kuanza CHAN kwa ushindi
KENYA Jumapili ilianza Kombe la Afrika kwa wachezaji wa nyumbani (CHAN 2024) kwa ushindi baada ya kuilemea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 1-0 katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani.
Bao hilo lilifungwa na kiungo wa Gor Mahia Austin Odhiambo kipindi cha kwanza baada ya mabeki wa DR Congo kushindwa kumsimamisha.
Stars walitawala mechi hiyo kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili waliwasoma wachezaji wa DR Congo huku wakivamia na kurejea nyuma.
Harambee Stars sasa inaongoza Kundi A kwa alama tatu kabla ya mechi kati ya Morocco na Angola baadaye katika uwanja wa Nyayo kuanzia saa 12 jioni.
Kufuatia ushindi huo, kila mchezaji wa Stars amejizolea Sh1 milioni alizoahidi Rais William Ruto. Kenya itacheza na Angola mnamo Alhamisi
Habari zaidi kufuata….