TIMU ya soka ya mabinti ya  Rising Starlets ya wachezaji chini ya miaka 20, inaingia siku yake ya sita ya mazoezi leo, kwa maandalizi ya  kupambana na Tanzania katika mechi mbili za raundi ya tatu za kufuzu Kombe la Dunia.

Starlets wataanza kampeni yao ya kufuzu nyumbani mnamo tarehe 7 mwezi ujao katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi, kisha mechi ya marudiano itachezwa siku saba baadae nchini Tanzania.

Mshindi wa jumla ya mabao atakutana na mshindi kati ya Cameroon na Botswana ambao watamenyana katika raundi ya tatu.

Kocha Jackline Juma jana, alitaja kikosi cha muda cha wachezaji 32. Awali aliita kambini wachezaji 60 ambao waliripoti kambini kutathmini ubora wao, utimamu wa mwili na mahitaji ya kimbinu ya benchi la ufundi.

Kufuzu raundi hii, Kenya ilipata ushindi wa 5-1 wa jumla ya mabao katika raundi ya pili dhidi ya Ethiopia. Mechi ya  mkondo wa kwanza iliishia sare ya 1-1 mjini Addis Ababa kabla ya kupata ushindi wa 4-0 nyumbani. Kenya ilipewa tiketi ya moja kwa moja kushiriki raundi ya pili.

Kwa upande mwingine Tanzania nao, waliinyeshea Angola 7-0 Jumla ya mabao (3-0, 4-0) katika raundi ya pili.

Kikosi cha muda cha kocha Juma, kina mseto wa wachezaji wenye uzoefu ambao walicheza raundi ya pili na ambao walivutia katika mazoezi ya siku tano.

Kukaa kwa siku tano kambini kumeruhusu benchi ya ufundi kuzingatia maandalizi ya kimbinu, viwango vya utimamu wa mwili, na uwiano wa timu kabla ya mechi hiyo muhimu.

Akizungumza jana baada ya mazoezi katika uwanja wa Kasarani Annex jijini Nairobi, kocha Juma anaelekeza nguvu zote kwenye changamoto inayoikabili Tanzania katika hatua hii ya kufuzu.

Kikosi cha Mda

Walinda lango

Christine Adhiambo, Mercy Akoth, Velma Abwire, Ephy Awuor

Mabeki

Sharlot Atieno, Jenevive Mithel, Triza Ekesa, Dorcas Glender, Diana Anyango, Elizabeth Ochaka, Lorine Ilavonga, Patience Asiko, Pauline Sylvia

Viungo wa kati

Brenda Awuor, Pearl Olesi, Lornah Faith, Halima Imbachi, Susan Akoth, Jerrine Adhiambo, Velma Awuor, Vidah Akeyo, Rebecca Odato, Fasila Adhiambo.