• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Rising Starlets kukaribisha Angola uwanjani Nyayo

Rising Starlets kukaribisha Angola uwanjani Nyayo

NA TOTO AREGE

TIMU ya soka ya wanawake ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Starlets, itakaribisha Angola uwanjani Nyayo mnamo Jumapili katika raundi ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake mwakani.

Mechi hiyo itaanza saa tisa alasiri.

Shirikisho la Soka nchini (FKF) lilitangaza kuwa kiingilia mechi hiyo kitakuwa bure.

Mshindi wa jumla wa mechi zote mbili atakutana na mshindi kati ya Cameroon na Botswana katika raundi ya tatu na ya nne baadaye mwaka huu 2023.

Mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia nchini Colombia kuanzia kati ya Septemba 5-22, 2024.

Kocha Beldine Odemba wa warembo wa Kenya alisema kikosi chake kiko imara.

“Pambano dhidi ya Angola ni kama kuenda vitani kupigania nchi. Tumejiandaa vizuri na wasichana wako tayari na nina matumaini tutafika raundi ya tano. Sijawasoma sana wapinzani wetu, lakini kutokana na mechi za awali nilizoziona, tunaweza tukawashinda,” alisema Odemba.

Kwa upande mwingine, Angola ilikumbana na kucheleweshwa kwa kupata visa zao, hali ambayo ilisababisha kuwasili kwao Kenya kuchelewa.

Licha ya kizuizi hiki, walifanikiwa kufanya mazoezi yao ya kwanza na ya pekee katika uwanja jioni ya Jumamosi.

Wakati Rising Starlets wanapanga kuwanyeshea Angola, nahodha Jane Nato amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwashabikia.

  • Tags

You can share this post!

Gesami akanusha madai alitaka Gavana Nyaribo amwage unga

Drama Mbeyu akipokonywa ‘mic’ kwa kulaumu...

T L