Dondoo

Adai huwachangamkia vidosho ili apate hanjam za kutawala ‘mechi’

Na JANET KAVUNGA April 9th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa aliwaacha wenzake kwa kicheko aliposema alimsuta mumewe vikali kwa kumfanya fala kwa kudai alichepuka ili kupata hanjam za kumpandisha mzuka chumbani.

Demu alisema aligundua jamaa alikuwa akichangamkia vipusa na kuwasiliana nao kwenye mitandao ya kijamii.

Alipomuuliza kwa nini alikuwa akisaliti kiapo cha ndoa yao, jamaa alidai lengo lake si kuchovya asali ya vidosho hao bali ni kupata hamu ya kuwika chumbani.

“Nilimwambia siwezi kukubali anifanye fala. Nilimpa onyo aachane na tabia hiyo au nimuache na kumsahau. Nusura apige magoti kuniomba msamaha,” demu alisema huku marafiki zake wakiangua kicheko.