Dondoo

Atishia kuvunja ndoa yake mume alipomuagiza ahame chama chenye vidume mafisi

Na JANET KAVUNGA February 1st, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa Mtopanga jijini Mombasa alitishia kuvunja ndoa yake baada ya mumewe kumtaka aache kutangamana na wanaume.

Tofauti zao zilianza buda alipogundua kuwa mkewe amejiunga na chama ambacho baadhi ya wanachama ni wanaume wanaojulikana kwa hulka ya kunyemelea wake wa watu.

Chama hicho ni kikundi cha kusaidiana, na mume huyo alikuwa amekataa kujisajili akisema hakutaka kutagusana na watu wasio na maadili mema.

Hata hivyo, juzi mkewe alijiandikisha kwa chama bila kumfahamisha mumewe ambaye aliwaka alipopata habari hizo na kumtaka ajiondoe mara moja.

Lakini mwanadada alikataa katakata na kutishia kumtaliki kalameni akimsuta kwa kujitenga na watu akijifanya yeye ni mwungwana sana.