Dondoo

Demu aliyekula ‘fare’ ajifungia chumbani polo alipomuandama hadi kwake

Na JOHN MUSYOKI February 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KIPUSA mmoja mtaani hapa alijifungia chumbani asiabishwe na jamaa aliyefika plotini kumtafuta baada ya kutafuna nauli aliyomtumia ili akamtembelee.

Inaarifiwa kuwa demu alimtaka jamaa amtumie nauli ili amtembelee na alipokosa kufanya hivyo, jamaa aliamua kumsaka.

Marafiki walimweleza jamaa kwamba kipusa huyo alikuwa ameonekana kwenye ploti na akaelekea huko.

Lakini demu kubaini anasakwa na jamaa, alijifungia ndani ya nyumba na kutulia tulii.

Jamaa alibisha mlango wa chumba cha demu na alipochoka, aliondoka kwa hasira huku akiapa kumchukulia demu huyo hatua.

“Endelea kula nauli na kujifungia ndani tu. Ipo siku tutapatana ana kwa ana. Lazima utarudisha hela zangu,” jamaa alisema akiondoka.