Demu aaachwa na mpenzi sababu ya kuropokaropoka
KIPUSA mmoja kutoka hapa alitemwa na mpenzi wake kwa kuropokwa sana.
Jamaa na demu walikutana kwenye sherehe moja ya harusi na wakawa marafiki.
Baadaye, wawili hao waliamua kukutana ili wajuane zaidi.
Inasemekana walipokutana walifurahi na kukumbatiana kwa muda huku demu akibubujikwa na machozi ya furaha kwa kuwa alitamani mwanamume wa kumchangamkia.
Pindi walipoanza kuzungumza, furaha ya jamaa ilitoweka kufuatia matamshi ya mwanadada huyo.
“Ni kweli wewe ni mrembo. Una umbo la kupendeza lakini matamshi yako hayana heshima hata kidogo,” jamaa alimwambia demu.
Hata hivyo, demu alishangazwa na matamshi hayo kwa sababu hakuona shida ya matamshi yake.
“Heri nikwambie ukweli. Mimi na wewe hatuwezi kuendelea kuchumbiana.
“Matamshi yako kwa kweli yanaweza kuniaibisha mbele ya watu.
“Pia tabia yako naitilia shaka,” jamaa alisema huku demu akiangua kilio.
Hata hivyo, huzuni wa demu huyo haukubadilisha uamuzi wa jamaa.