Dondoo
Jombi adai alipapaswa na demu kwenye treni
MWANAMUME mmoja amewashangaza wengi baada ya kuripoti kuwa alinyanyaswa kingono na mwanamke aliyekuwa akipita karibu na kiti chake ndani ya treni.
Kisa hicho kilitokea hadharani, jambo lililozua mjadala mpana kuhusu unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanaume.
Polisi wametoa picha za CCTV wakimtaka mwanamke huyo ajitokeze au kusaidia katika uchunguzi. Maafisa wamesisitiza kuwa unyanyasaji wa kingono, bila kujali jinsia, ni kosa kubwa la jinai.
Wanaharakati wametoa wito kwa waathiriwa wote kuripoti visa kama hivyo bila woga.