Dondoo

Jombi amchoka mke damu moto aliyezoea kuligawa tunda mtaani

Na JANET KAVUNGA April 15th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MAKUPA, MOMBASA

KALAMENI mmoja wa hapa aliwaka kwa hasira alipogundua kuwa mkewe hakuacha kugawa tunda licha ya kumsamehe mara mbili kwa kuchepuka.

Demu ana damu moto ajabu na mumewe alimfumania mara mbili akitoka gesti na kumsamehe.

Kila wakati aliosamehewa, demu aliahidi kuacha tabia hiyo.

Hata hivyo juzi, mumewe alimpata akiwa na polo mmoja wakitoka gesti na akaudhika mpaka akashindwa kujizuia.

Alimfokea vikali kwa kuendelea kumuaibisha mtaani kwa tabia yake ya uzinifu na kumtaka asikanyage kwake.

“Nimekuvumilia vya kutosha na hii tabia yako. Kuanzia sasa, usitie guu kwangu. Naenda kuchoma chochote kinachonikumbusha wewe. Endelea na tabia yako ya umalaya,” jamaa aliwaka huku polo aliyekuwa gesti na demu akipiga kona na kutoroka.