Kalameni akosa mistari kidosho alipokiri kinachomvutia ni pesa, si huba
POLO aliyekuwa akimezea mate demu mmoja aliingia baridi mwanadada huyo alipomwambia wazi kuwa anapenda pesa sana.
Jamaa alikuwa akirushia demu mistari ya mapenzi na siku moja binti akampa miadi wakutane katika hoteli moja.
Walipokuwa wakipiga gumzo wakiendelea kuteremsha vinywaji, demu alisema yeye anapenda pesa sana na anaweza kufanya chochote kuzipata.
“Siwezi kuacha pesa. Ninaweza kufanya chochote mradi tu nizipate kisha nishughulikie athari zinazofuata baada ya kuziweka mfukoni,” demu alisema.
Jamaa alipomdadisi zaidi, demu alishikilia kuwa hawezi kuvumilia mwanamume bila pesa.
“Hii ndiyo sababu siwezi kujifunga kwa mwanamume mmoja kwa kuwa akiishiwa lazima nitamtema niende kwa aliye nazo,” demu alisema na jamaa akaamua kuachana naye.