Kalameni kwenye fumanizi akwama dirishani akitoroka
HANGZHOU, China
TUKIO la kushangaza na la aibu lilishuhudiwa katika mji huu baada ya jombi kunaswa kwenye video akining’inia kwenye roshani ya hoteli akiwa amevaa boksa pekee.
Inasemekana mwanaume huyo alikuwa akijaribu kutoroka kupitia dirisha ili asionekane baada ya kudaiwa kufumaniwa akila uroda chumbani na mke wa mtu.
Walioshuhudia walisema mwanaume huyo aliteleza na kujikuta akining’inia juu ya roshani ya hoteli, akishindwa kupanda wala kushuka.
Video za tukio hilo zilisambaa kwa kasi mitandaoni na kusababisha kicheko na kejeli kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hatimaye, maafisa wa zimamoto waliingilia kati na kumshusha salama.
Polisi walisema hakuna aliyekamatwa, lakini tukio hilo limeacha maswali mengi kuhusu uhusiano wa siri na maamuzi hatari yanayochukuliwa baada ya kufumaniwa katika michepuko.