Dondoo

Kidosho aliyepata mimba baada ya michepuko arudi kwa wazazi kiaibu

Na JOHN MUSYOKI November 13th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

KIPUSA mmoja aliyeolewa hapa alirudi kwa wazazi wake baada ya kupata mimba nje ya ndoa.

Penyenye zinasema kuwa demu huyo alikuwa na mpango wa kando huku mumewe akiishi Thika anakofanya kazi.

Mwezi jana, mumewe alifika nyumbani bila kutarajiwa, hali iliyomtia demu kiwewe na akaamua kurudi kwa wazazi wake, uamuzi ambao ulishangaza kwa sababu walijua alikuwa mjamzito.

“Kwa nini unataka kuondoka na tayari wewe ni mjamzito? Kwani kuna shida gani? Umekosana na mumeo?” mama mkwe alimuuliza.

“Mimi ninaenda kwa sababu sitaki kisirani,” demu alisema na kuondoka na baadaye mumewe akasema mimba haikuwa yake.