Mamapima audhi wateja kudai binti yake hawezi kabisa kuolewa na mlevi
KIOJA kilizuka katika boma la mamapima wa eneo la Nyamachaki, Nyeri baada ya wateja wake kumfokea kwa kuwadharau.
Inadaiwa kwamba makalameni waliokuwa wakiburudika kwa mamapima waliudhika baada ya mamapima kudai binti wake hawezi kuolewa na mlevi.
“Acha madharau. Sisi walevi ndio tunaojua kukaa na wanawake. Lazima utupe heshima,” mamapima alionywa.
Mamapima aliwakemea walevi hao huku akidai anajua tabia ya kila mmoja wao.
“Nyote nawajua. Mkilewa mnakuwa watu ovyo sana. Msichana wangu ana akili. Anahitaji mtu mwenye akili kama zake,” mamapima alifoka.
Makalameni walitishia kuondoka lakini vitisho vyao havikumshtua mamapima.