Dondoo

Mwanamume alipia mtoto wa demu aliyemkataa karo ya mwaka mzima

Na JANET KAVUNGA February 19th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa amebaki na maswali mengi jombi aliyemkataa kwa sababu ya umasikini, alipomlipia binti yake karo ya shule ya mwaka mzima.

Demu alitemwa na mwanamume aliyemuoa baada ya kumkataa jamaa huyo ambaye baadaye aliomoka akawa anamezewa mate na wanawake wakiwemo walioolewa.

Juzi, jamaa alipata habari kwamba, binti ya mwanadada aliyemkataa hakuwa amerudi shule kwa kukosa karo.

Alienda katika shule akalipa karo ya mwaka mzima na akaagiza mwalimu mkuu ampigie simu mama wa msichana amweleze karo ilikuwa imelipwa yote.

Ni wakati alifika shuleni alipofahamishwa ni jamaa aliyelipa karo na kwa sasa ameshindwa jinsi ya kumfikia amshukuru kwa kuwa hana simu yake na hajui anakoishi.