Dondoo

Mwenye teksi ashtumu mteja kwa kumpeleka kwa mganga

Na JANET KAVUNGA April 30th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

DEREVA wa teksi alimfokea mteja wake kwa kumdanganya kwamba safari yake kwenda Kinango ilikuwa ya kutembelea wazazi ilhali alikuwa akienda kwa mganga.

Dereva huyo ambaye ni mlokole alisema kwamba, alikasirika walipofika kwa boma la mganga.

“Tukiwa Mombasa aliniambia alikuwa akienda nyumbani kuona wazazi wake. Hata hivyo, boma alilonielekeza lilikuwa la mganga na kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakisubiri kuhudumiwa. Nilikasirika kwa kuwa sipendi mambo ya waganga na kama angenieleza ukweli ningekataa kwenda,” alieleza dereva huyo akitoa ushuhuda katika mkutano wa maombi kwa rafiki yake.

Alisema nusura amuache lakini akavumilia huku akiendelea kumuombea aweze kuona nuru na kuacha kuamini nguvu za giza.