Pasta aanika kidosho muumini aliyekula ‘fare’ yake wakati akimtongoza
PASTA wa kanisa moja mjini Thika alishangaza waumini alipoanika demu aliyekula ‘fare’ nyingi alipokuwa akimtongoza.
“Ala, kumbe umetutembelea kanisani? Huyu mrembo nilimtongoza kitambo. Shida ni kwamba alikula fare yangu nyingi na hakuna siku hata moja aliwahi kunitembelea. Hata hivyo, nashukuru Mungu aliolewa na ametulia,” mchungaji alisema huku waumini kanislani wakiangua vicheko.
Demu alipopewa kipaza sauti alikiri kwamba pasta aliwahi kumtongoza siku za ujana wao.
“Ni kweli mtumishi wa Mungu alikuwa akinitaka lakini sikuwa tayari. Nilipenda jinsi alikuwa mkarimu. Kweli ksabisa alikuwa akituma fare nami natafuna tu,” mwanadada alikiri.
“Ninashukuru kwa sababu ana mke na watoto na mimi nina mume na familia,” kidosho aliongeza huku akijumuika na wengine katika kicheko.
Mchungaji huyo, hata hivyo, alishauri vijana wasikasirike vipusa wakila ‘fare’ lakini pia akaonya vidosho dhidi ya tabia hiyo.
“Heri uambie mtu humpendi badala ya kula pesa zake bure, hiyo ni laana,” pasta alieleza.