• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Polo ashirikiana na wezi kwake kuporwe

Polo ashirikiana na wezi kwake kuporwe

Na BENSON MATHEKA

MAKADARA, ATHI RIVER 

WAKAZI wa mtaa huu walifurahia sinema bila malipo mwanadada alipomgombeza mumewe akimlaumu kwa kupanga njama nyumba yao ivunjwe na mali kuibwa.

Duru zinasema jamaa na mkewe hawakuwa wakiishi kwa amani kwa muda. “Ndoa yao ilivurugika mwanadada alipompata jamaa peupe akiwa na mpango wa kando.

Kuanzia siku hiyo, jamaa alijaribu kumfukuza mkewe lakini mwanadada alikataa kuondoka,” alisema mdokezi. Siku ya kioja, jamaa alikuwa kazini na mkewe akawapeleka watoto wao shule.

Aliporejea alikuta mlango wa nyumba yao ukiwa wazi na akadhani ni mumewe aliyerejea kutoka kazini. Hata hivyo, alipoingia ndani, aligundua kuwa vifaa kadhaa kama vile redio, runinga, mtungi wa gesi, pasi na nguo hazikuwemo.

“Kilichomjia akilini ni kuwa ni mumewe aliyepanga vitu hivyo viibwe au aliyevichukua na kuhama kwa sababu ya kuvurugika kwa uhusiano wao.

Alipompigia simu, jamaa hakuonekana kushangaa na demu akawa na imani kwamba ni mumewe aliyepanga njama nyumba ivunjwe na mali kuibwa,” alisema mdokezi.

Yasemekana mumewe ambaye kusema kweli hakufahamu aliyeiba mali yao alipotoka kazini, mkewe alianza kumgombeza hata kabla ya kuingia ndani ya nyumba.

“Hautaingia hapa bila vifaa ulivyotumana viibwe. Najua ulimtuma mpango wako wa kando kuiba kama njia ya kunifukuza lakini hauna bahati, nenda ukamwambie havirudishe, “ mama aliwaka.

Inasemekana jamaa alipojaribu kuingia ndani ya nyumba, mwanadada alifunga mlango na akaendelea kuropokwa maneno machafu ambayo hatuwezi kuchapisha hapa.

Kulingana na mdokezi, watoto walianza kulia wakitaka kumuona baba yao ndipo mwanadada akamfungulia jamaa mlango.

Haikubainika kilichomfanya demu kutuliza hasira lakini siku iliyofuata, alionekana kuaibika kwa tabia yake ya kumkosea heshima mumewe.

 

You can share this post!

Serikali yaunda kamati kukabiliana na konokono

CORONA: Wakenya sasa waambukizana

adminleo