Dondoo
Slayqueen atema polo baada ya kazi kuisha
JOMBI kutoka hapa Makutano mjini Mwala, Kaunti ya Machakos, aliachwa kwa mataa mpenzi wake alipomtema baada ya kuuza gari lake kazi ilipoisha.
Duru zinasema mwanamume huyo aliuza gari baada ya kupoteza kazi ili akidhi mahitaji mengi ya kidosho.
“Tuko hali ya kuvumiliana. Nivumilie na nina hakika kwamba hivi karibuni mambo yatakuwa shwari,” polo alimsihi mwanadada.
Lakini demu akamrushia mikono na kujibu: “Uvumiliwe na nani kama huna pesa? Kama hakuna pesa itabidi ukae peke yako. Siwezi kuvumilia uhusiano ambao hauna mbele wala nyuma.”