‘Tattoo’ za kutisha katika mwili wa polo zatibua mpango wake wa kula uroda na demu
MATARAJIO ya demu kufurahia miadi na polo mmoja wa Nyali jijini Mombasa yalizimika mwanadada alipoingizwa baridi na ‘tattoo’ za kutisha kwenye mwili wa jamaa huyo.
Wawili hao walikuwa wamekutana kwa miezi kadhaa kufahamiana kabla ya kuamua kutia muhuri uhusiano wao kwa kulishana asali.
Walikutana katika gesti moja mtaani hapa kila mmoja akiwa na hamu ya kufurahia siku hiyo lakini demu akashtuka polo alipovua shati na akaona michoro ya ajabu katika mwili wa jamaa.
“Alikuwa na michoro ya kutisha ya nyoka na mifupa mwilini. Nilishtuka hadi hamu ya kulishana asali ikaisha. Nilipiga nduru akashtuka pia. Nilichomoka chumbani na huo ukawa mwisho wa uhusiano wangu naye,” demu alieleza mademu waliokuwa wakibadilishana uzoefu wao kuhusu matukio ya kushtua kwenye mahusiano ya mapenzi.