Usiniletee mchezo kwenye biashara, kipusa awakia polo aliyedhani amepata penzi la dhati
POLO kutoka mtaa mmoja mjini hapa alijuta baada ya kupigwa na demu aliyedhani ni mpango wa kando.
Inasemekana jamaa alikutana na kipusa huyo mtandaoni, wakawasiliana kwa muda kabla ya kupanga wakutane katika hoteli moja.
Baada ya kuburudika katika gesti kwa saa kadhaa, demu alitarajia jamaa ampe pesa lakini akamkausha.
Mwanadada alipandwa na hasira na akampapura jamaa bila huruma akimwambia hafai kucheza na kazi yake.
Hapo ndipo jamaa aligundua kwamba mwanadada huyo alikuwa hawara maarufu anayetumia mitandao ya kijamii kupata wateja akiwahadaa eti anasaka wapenzi.
Polo sasa anasema hatarudia tena michezo ya kando, akisema afadhali akae na mkewe kuliko kuwekeza kwa matapeli wa mapenzi.