• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:55 AM
Cofek yapinga benki kupewa uhuru wa kudhibiti viwango vya riba

Cofek yapinga benki kupewa uhuru wa kudhibiti viwango vya riba

Na RICHARD MUNGUTI

SHIRIKISHO la watumiaji wa bidhaa (Cofek) Jumatatu liliwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa kuruhusu benki kutoza riba za juu kwa wanaokopa pesa.

Wakili Henry Kurauka alisema Cofek inapinga idhini iliyopewa benki kuwatoza wanaokopa pesa viwango vya juu vya riba.

Bw Kurauka alisema hatua ya kuzipa benki fursa ya kuamua kiwango cha riba inatatanisha. Amesema majaji hao walipata vipengee vya sheria za benki zinazua utata na kuvifutilia mbali.

Vipengee vilivyopatikana viko na utata ni nambari 33B(1) na (2) vya benki. Cofek iliwasilisha rufaa hiyo ya kupinga uamuzi wa majaji watatu wa mahakama kuu uliotolewa Machi 18, 2019.

Katika arifa aliyowasilishwa katika mahakama kuu, Bw Kurauka amesema kuwa uamuzi huo wa majaji hao watatu haujafafanua kwa uwazi kitakachojiri.

“Bila shaka wananchi wa kawaida wataathiriwa na uamuzi huo wa majaji hao wa watatu wa kuzipa benki fursa ya kuamua kiwango cha riba kitakachokuwa kinatolewa,” asema Bw Kurauka.

Alisema atawasilisha rufaa kabla ya siku 60 kukamilika akiomba mahakama hii ya pili kwa ukuu ibatilishe uamuzi wa kuzipa benki uhuru wa kuamua riba itakayowatoza wanaopokea mikopo.

Majaji Francis Tuiyot, Jacquiline Kamau na Rachel Ng’etich waliruhusu benki kuamua kiwango cha riba cha kuwatoza wanaopokea mikopo.

Hatua hii ya kuruhusu benki kuweka viwango vya riba ilijadiliwa na bunge kisha zikapewa uhuru wa kuweka riba itakayotozwa wananchi.

Bunge liliidhinisha benki kutoza asilimia 70 iliyowekwa na Benki kuu ya Kenya (CBK) na kuamuru kiwango cha chini kabisa kilichowekwa kuwa asilimia 6.3.

Mahakama ilifahamishwa kuwa iwapo benki zitakubaliwa kuweka viwango vya riba basi wawekezaji wanaotegemea mikopo wataathiriwa pakubwa.

You can share this post!

Dhamana ya Sh50,000 kwa kujifanya Jaji Ibrahim

MAPOZI: Eddie Butita

adminleo