Wanafunzi walio nyumbani watayarishwe kurudi shuleni – Magoha
NA FAUSTINE NGILA
Waziri wa Elimu George Magoha amewaomba wazazi waanze kuwatayarisha wanafunzi walio nyumbani kurudi shuleni wiki mbili zijazo.
Hii ni baada ya shule kufunguliwa leo darasa la nane , nne na kidato cha nne kwa muhula wa pili.
Alipokuwa akifanya ukaguzi wa matayarisho ya shule kwenye shule ya msingi ya Olympic waziri huyo aliwaomba wazazi kutayarisha wanao kwa masomo.
“Wizara ya elimu itachunguza hali hiyo wiki moja au mbili ndio waite wanafunzi wengine shule. Aliwaomba wazazi wasiwe na hofu kuhusiana na usalama wa watoto wao.
“Isipokuwa kwa wanafunzi ambao wanamagonjwa mengine matembezi ya shuleni yanapaswa kuachwa,”alisema. Aliwaomba wazazi ambao wanamagonjwa mengine wajulishe shule.
Alizitaka shule kutengeneza kamati za kukabiliana na corona na pia mikutano na michezo kwanza isitishwe. Aliwaomba pia wanafunzi walio na mimba kurudi shuleni
“Wanafunzi wetu wakirudi shuleni wanapaswa kuwekwa kwenye mazingira mazuri,” alisema.