Afisa aliyeghushi stakabadhi apigwa faini ya Sh200,000
BRIAN OJAMAA na FAUSTINE NGILA
AFISA wa kaunti ya Bungoma alipigwa faini ya Sh200,000 kwa kukosa kufika kortini kusikiza mashtaka yake ya kutumia stakabathi gushi.
Jonathan Chenjeni,ambaye anafanya kazi kwenye ofisi ya Gavana Wycliffe Wangamati aliwasilisha stakabathi gushi kwa karani wa bunge hilo John Mosongo mwezi uliopita.
Stakabathi hiyo ilikuwa ni barua iliyoonyesha kwamba swala ya kumng’oa mamlakani Bw Wangamati lilikuwa limetupiliwa mbali.
Walalmikaji mabao ni wananchi wa Bungoma wanataka gavana huyo atolewe kwa sababu ya utumizi mmbaya wa mamlaka.
Mwenyekiti wa kamati hio ya uogozi na maswala ya mitandao Henry Okumuu Majimbo alimpa faini hio Bw Chejeni baada ya kukosa kufika kujibu maswala kuhusiana na stakabathi hizo gushi.
“Stakabathi hio ya kufogi ilionyesha kwam ba Moses Lukoye mlalamikaji mmoja alikuwa ametupilia mbali lalamishi yake .Bw Lukoye alikana kwamba aliandika stakabathi hio,” alisema bw majimbo.
Meshack Museveni, mwanachama wa kamati hio alisema kwamba Bw Chenjeni alikuwa amehojiwa kutokana na makosa mengine.