• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Afisa wa itifaki wa Sakaja asaidia wasichana wawili kuingia Kidato cha Kwanza

Afisa wa itifaki wa Sakaja asaidia wasichana wawili kuingia Kidato cha Kwanza

NA SAMMY KIMATU

WASICHANA wawili werevu kutoka katika familia maskini zenye makazi Mukuru katika tarafa ya South B, Kaunti ndogo ya Starehe sasa wana furaha baada ya afisa wa itifaki wa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, Bw Rodriques Lunalo, kuingilia kati kuwawezesha kujiunga na Kidato cha Kwanza.

Elizabeth Awuondo aliyefanya Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE 2023) katika Shule ya Msingi ya St Catherine na kupata alama 371 na akapata ufadhili wake wa masomo kutoka kwa kampuni ya kuoka mikate ya Broadway mjini Thika.

Mwanafunzi mwingine kwa jina Kimberly Nkatha aliyepata alama 403 alikwama lakini karo yake ikagharimiwa na gavana Sakaja.

Sasa Elizabeth yuko Mary Hill School Thika huku Nkatha akijiunga na Arya Girls.

Bw Rodriques Lunalo alipompeleka Elizabeth Awuondo shuleni Mary Hill School Thika. PICHA | SAMMY KIMATU

Hapo awali, Bw Lunalo alikuwa kiongozi wa vijana katika maeneo ya South B kwa zaidi ya mwongo mmoja.

“Ninatoka katika mtaa wa mabanda. Tuna watoto werevu, vijana wenye talanta lakini changamoto kuu katika mitaa ya mabanda ya Mukuru ni umaskini wa kupindukia unaochangiwa na ukosefu wa ajira kwani wakazi wengi wa Mukuru walipoteza kazi katika eneo la Industrial Area walikofanya kazi kama vibarua,” Bw Lunalo akasema.

  • Tags

You can share this post!

Papa adai wanaopinga mashoga wana unafiki

VAR yaongeza ladha ya Afcon

T L