• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 4:07 PM
Afueni bei ya nyanya ikishuka ghafla

Afueni bei ya nyanya ikishuka ghafla

Na VICTOR RABALLA

NI afueni kuu kwa wanunuzi bidhaa Magharibi mwa Kenya kufuatia kushuka ghafla kwa bei za nyanya huku wachuuzi wakifurika taifa jirani la Uganda kuziba upungufu.

Katika kipindi cha chini ya wiki tatu, bei ya bidhaa hiyo imeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 kulingana na Mwenyekiti wa Kundi la Wauzaji Nyanya Kisumu BwTom Justo.

Kwa sasa, alisema wauzaji bidhaa wanauza nyanya kwa bei ya jumla ya Sh6,000 kutoka kwa Sh15,000 kwa kreti moja katikati mwa mwezi uliopita.

“Jambo hili limefanya bei za nyanya katika eneo hili kurejelea hali ya kawaida,” alieleza Taifa Leo jana.

Alieleza kwamba bei ya zao hilo huenda ikashuka zaidi hadi kati ya Sh3,000 na Sh4,000 katika kipindi cha mwezi mmoja ujao huku vua kubwa zikitarajiwa kupungua.

Bw Justo alisema bado kuna upungufu wa bidhaa hiyo Kenya ambapo kiwango kilichopo hakiwezi kutosheleza wateja, hivyo kufanya wafanyabiashara kuagizia bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima wa Uganda.

“Wakulima wa Kenya bado hawajarejelea hali yao ya kawaida baada ya kupata hasara kuu kutokana na uharibifu uliosababishwa na vua kubwa zilizoshuhudiwa katika maeneo kadha kote nchini,” alisema.

Mfanyabiashara huyo alifafanua kwamba zao hilo nchini Kenya liliathiriwa pakubwa na ugonjwa ambao ni hatari zaidi miongoni mwa maradhi yote ya nyanya.

Ugonjwa huo husababishwa na wadudu wanaoenea katika mmea wa nyanya hasa wakati wa msimu wa unyevunyevu na husambaa kwa kasi huku ukisababisha matawi kukauka, kuoza na kuanguka.

Kutokana na uhaba wa nyanya sokoni, wakazi Kisumu walilazimika kununua nyanya kwa bei ya hadi Sh30 katika soko mbalimbali kama vile Kibuye, Kondele na Ahero.

  • Tags

You can share this post!

Igathe njiani kwa cheo chake cha naibu gavana?

Kiwanda chatimua watu 280

adminleo