Habari Mseto

Ageuza jumba lake kuwa makao ya wazee

October 7th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA MERCY MWENDE

Mwanamume wa miaka 94 Nduhiu Njama ameanzisha mpango wa kuwasaidia wazee kutoka kaunti ya Nyeri.

Kwa kugundua kwamba vijana wote wamehamia mijini kutafuta kazi huku wazee wakiachwa bila watu wa kuwachunga, ameamua kufanya jumba lake ambalo amelijenga kwenye shamba la hekaeri sita makao ya wazee.

Sababu ya kufanya hivi ni kwamba kazi ya Watoto ya kuwachunga wazee imebailika huku wazee wakihitaji Maisha nzuri siku zao za uzeeni.

Bw Njama ambaye ni mwalimu mkuu mstaafu na baba ya Watoto sita aliamua kufanya jumba hilo la thamani ya  Sh6 milioni alilojenga mwaka wa 1992 kijijini Kiawaithanji, eneobunge la Tetu kuwa makao ya wazee.

“Kabla ya mke wangu kufariki mwaka wa 2003 tulikuwa tumepanga kuisaidia jamii. Lakini kwasababu sasa hayupo, sina mtu wa kugawa naye mali yangu baada ya kustaafu,” Bw Njama aliambia Taifa Leo Jumatano..

Mwaka 2015 Bw Njama alisajili kituo cha kuokoa wasichana ambao hawamudu kulipa karo ya shule ya upili ilioyojiita “Gladys and Njama Foundation”.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA