• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Akana kuondoa jina la katibu kwa kesi ya transfoma

Akana kuondoa jina la katibu kwa kesi ya transfoma

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA mkuu katika idara ya ununuzi wa mali ya serikali (PPRA) Bw Linus Muriithi alikanusha kuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) , Bw Geoffrey Kinoti hakumwagiza aondoe jina la katibu mkuu Wizara ya kawi Joseph Njoroge katika ripoti ya ununuzi wa transfoma feki.

Bw Muriithi alimweleza hakimu mwandamizi Bw Felix Kombo kuwa hakuagizwa na DCI kutoa jina la Bw Njoroge.

“Je, uliamriwa utoe jina la Katibu mkuu Njoroge katika ripoti mliyoandaa kuhusu ununuzi wa transfoma na kampuni ya Muwa Trading Company Limited?” kiongozi wa mashtaka Bw Alexander Muteti alimwuliza Bw Muriithi.

“Sikuamriwa na mtu kutoa jina la Bw Njoroge,” alijibu Bw Muriithi.

Shahidi huyo alisema kuwa alifanya uchunguzi jinsi kampuni ya Muwa ilivyoteuliwa kununulia kampuni ya Kenya Power (KP) zaidi ya transfoma 300 kutoka ng’ambo.

Alisema Muwa iliteuliwa siku 90 baada ya muda kuyoyoma wa uteuzi.

Alisema alipata kasoro nyingi sana katika uteuzi huo kwa vile kamati ya ufunguzi wa tenda haikuwa imeteuliwa kwa njia ipasayo.

Bw Muriithi alisema hayo alipotoa ushahidi katika kesi ambapo waliokuwa wakuu wa KP Dkt Ben Chumo na Dkt Ken Tarus wameshtakiwa kwa ufujaji wa zaidi ya Sh400milioni.

Kesi inaendelea.

  • Tags

You can share this post!

Majabali wa KCSE 2018 watajwa

Nimetii masharti yote ya mahakama, asema Obado

adminleo