• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Anayeshtakiwa kuiba moyo wa maiti aomba kesi ifutwe

Anayeshtakiwa kuiba moyo wa maiti aomba kesi ifutwe

Na RICHARD MUNGITI

ALIYEKUWA mpasuaji mkuu wa maiti wa Serikali, Dkt Moses Njue anayeshtakiwa pamoja na mwanawe kwa wizi wa moyo kutoka kwa maiti Jumatatu waliwasilisha kesi katika mahakama kuu wakiomba kesi hiyo ifutiliwe mbali.

Dkt Mureithi Njue na Dkt Lemuel Anasha wanaomba mahakama kuu imzuie Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) wakidai hakuhoji sheria ipasavyo kabla ya  kuagiza wafunguliwe mashtaka ya kuiba moyo wa maiti.

Katika kesi iliyowasilishwa chini ya sheria za dharura , Dkt Njue anasema haki zake kikatiba pamoja na za mwanawe zimekandamizwa na DPP.

Wawili hao wanaomba mahakama kuu iingilie na kusitisha mara moja kesi waliyoshtakiwa Mei 15 , 2018 isitishwe kusikizwa hadi kesi hii isikizwe na kuamuliwa.

Dkt Njue na mwanawake wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kuiba moyo. Dkt Njue alifikishwa kortini mnamo Mei 15 lakini mwanawake Lemuel hakufika.

Bw Andayi alimwamuru Lemuel afike kortini kabla ya siku ya kusikizwa kwa kesi ajibu mashtaka.

Lemuel aliagizwa afike kortini mnamo Julai 3,2018 kujibu shtaka.

Katika kesi waliyowasilisha kortini wawili hao wanasema katiba inakataza mtu kufunguliwa mashtaka kabla ya kuhojiwa kwa dhati sheria na katiba kubaini ikiwa haki za mshukiwa zimetwezwa.

Dkt Njue na mwanawe walifunguliwa mashtaka ya kuiba moyo wa Timothy Mwanzi jana alishtakiwa kwa kuiba moyo wa maiti katika Mochari ya Lee, ilioko Nairobi Hospital.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Bw Noordin Hali aliwasilisha mashtaka matatu dhidi ya Dkt Njue ya kuiba moyo Timothy Mwandi Muumba.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka matatu ya kuiba moyo, kuvuruga ushahidi na kuondoa kiungo katika maiti lakini akaachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 pesa tasilimu.

Alikabiliwa na mashtaka ya kuiba moyo kutoka kwa mwili wa Timothy Mwandi Muumba uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha Lee.

Na wakati huo huo, hakimu mkuu katika Mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi alitoa kibali cha kumwagiza Dkt Lemuel Anasha Mureithi Njue afike kortini   mnamo Julai 3, 2018 kujibu mashtaka matatu.

Juhudi za Dkt Njue, kupitia kwa mawakili wake kupinga asishtakiwe ziligonga mwamba baada ya Bw Andayi  kutupilia mbali ombi la kutaka kesi hiyo iahirishwe hadi Mahakama Kuu itakaposikiza na kuamua ombi  lililowasilishwa na jamaa wa marehemu.

Lakini ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa Serikali Bi Cathertine Mwaniki aliyesema kesi iliyowasilishwa 2016  ilipania kushinikiza afisi ya DPP ichunguze kisa hicho.

“Uchunguzi ulifanywa na idara inayohusika na mizozo ya kinyumbani katika afisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Jinai (DCI).

You can share this post!

Afisa wa Harambee Sacco akana kuiba mamilioni

Huenda kifungo cha maafisa waliomeza hela za makaburi...

adminleo